MICRON WAIJAZA YANGA MAPESA

Na Said Ally
Klabu ya Yanga leo hii imeingia mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi bilioni mbili na kampuni ya vifaa vya michezo ya Macron kwa ajili ya utengezaji na usambazaji wa jezi za klabu hizo.

Akiongea katika utiliani saini wa mkataba huo,katibu mkuu wa klabu ya Yanga Charse Boniphace Mkwasa alisema kwamba kwa sasa wafanya biashara wa jezi feki wanatakiwa kuacha mara moja kwani wahusika wa tenda hiyo hawatakuwa na mzaa kwenye swala hilo.

Alisema kwamba awali klabu ilikuwa haipati faida yeyote kwenye mauzo ya jezi kutokana na wafanya biashara kuuza jezi feki ambapo kwa sasa baada ya makubaliano hayo ya mkataba utakaokuwa na nyongeza katika kipindi cha miaka mitatu utaleta chachu ya kusaidia uendeshaji wa timu.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilishawahi kuvaa jezi zenye nembo ya Macron kampuni yenye makao makuu yake nchini Itali wakati waliposhiriki mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya timu ya Mo Bejaia.

No comments