TFF YASEMA MCHEZAJI WA MBAO HAKUPELEKWA NA GARI LA ZIMAMOTO
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.limesikitishwa na taarifa zinazoelezwa na baadhi ya watu zikidai kuwa shirikisho hilo limefanya uzembe wa kutozingatia kuweka gali la wagonjwa katika mchezo wa jana kati ya Mwadui na Mbao FC uliochezwa mkoani Kagera,mchezo uliosababisha kifo cha mchezaji Ismail Khalifani
Lucas amesema kwamba kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakitoa taarifa ambazo si za kweli hasa wakidai kuwa mchezaji ampelekwa hospitali kwa kutumia gali la zimamoto.
"Kuna nia ovu ya kutaka kujenga hoja kwamba TFF haikusimamia vyema,hiyo ndio nia ovu na wanaoneza hayo wa lengo la kuonyesha kwamba taasisi ina uongozi wa ovyo"alisema Lucas.
Lucas amesema kwamba taarifa hizo si za kweli kwani gari ambalo limetumika kumpeleka hospita ni gari ya wagonjwa wala sio ya zimamoto kama inavyoelezwa na wadau hao.
Hata hivyo vyanzo mbalimbali vya habari ambavyo vimeshuhudia tukio hilo vimethibitisha kuwa marehemu Ismail Khalifan alipelekwa kwa hospitali kwa kutumia gari ya zimamoto.
Post a Comment