MARTIN SAANYA NA MPENZU WAONDOLEWA KUCHEZESHA LIGI KUU

Waamuzi ambao wamechezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba,Martin Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye ratiba ya ligi kuu ya Tanzania bara,huku suala lao likipelekwa kwenye kamati ya waamuzin ili ishughulikie tatizo lao kitaalam.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba maamuzi hayo yamefanyika baada ya kikao cha kamati ya uendeshaji ya bodi ya ligi,kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika ambapo kamati imeibaini mapungufu mengi ya kiutendaji na waamuzi hao.

Pia mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha mchezo namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga nae ametolewa kwenye ratiba ya ligi kuu kwa msimu huu wa mwaka 2016/2017 na kurudishwa kwenye kamati ya waamuzi ili waweze kumpangia daraja linguine la uamuzi.

Lucas amesema kwamba kamati husika imebaini kuwa Mrope ameshindwa kujiamini mchezoni na kwenye uamuzi wake na kushindwa kuudhibiti mchezo.

Amesema kwamba miongoni mwa matatizo ya mwamuzi ni kukubali goli,kisha kukataa na mwisho kukubali tena hali iliyoonyesha kutojiamini na kusababisha mtafaruku mkubwa katika mchezo huo.

No comments