AKILIMALI AUNGANA NA UONGOZI JUU YA SWALA LA MBUYU TWITE

Katibu wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga,Ibrahim Akilimali amekubaliana na hatua iliyochukuliwa na uongozi ya kuachana na mchezaji Mbuyu Twite baada ya mchezaji huyo mkataba wake kuelekea ukingoni.

Akilimali amesema kwamba kwa upande wake kama katibu wa baraza la wazee anakubaliana na swala hilo kwani mchezo huyo umri wake ni mkubwa ambao hana muda mrefu katika ushiriki wa mpira wa miguu.

"Mimi nakubaliana na uongozi kabisa kwa hili kwani Mbuyu Twite umri ushakwenda hivyo naamini ni wakati wa kuiacha Yanga kwa sasa"alisema Akilimali.

Amesema kwamba pia yeye anaendelea na msimamo wake ule ule wa kutoridhishwa na kiwango cha mchezaji Obrey Chirwa na endapo kama uongozi utamtoa kwa mkopo mchezaji huyo utakuwa umefanya jambo zuri kwani kiwango chake hakistahili kuwepo ndani ya klabu ya hiyo ya Yanga.

No comments