TFF YAPOKEA KWA MAJONZI TAARIFA ZA KIFO CHA MCHEZAJI WA MBAO

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF chini ya raisi Jamali Malinzi,limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha kushtukiza cha mchezaji Ismail Halfan wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Ilemela jijini Mwanza kilichotokea siku ya jana ya tarehe 4 ya mwezi Disember kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.


Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba kifo cha mchezaji huyo ni pigo kubwa kwa Taifa kwani marehemu alikuwa na msada mkubwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

Lucas amesema kwamba kufuatia kifo hicho Shirikisho linaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakisha kuwa taratibu zote za mazishi zinakamilika kwa kushirikiana na familia ya marehemu pamoja na wadau mbalimbali na kwa upande wao wamewasilisha rambirambi ya shilingi laki tano.

Amesema kwamba kwa sasa wanasubiri ripoti ya madaktari kufahamu nini sababu ya kifo cha mchezaji huyo ili kuweza kuufahamisha uma wa watanzania juu ya jambo hilo.

No comments