KATIBU YANGA YANGA AMZUNGUMZIA MBUYU TWITE KWENYE MECHI DHIDI YA JKU

Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara,timu ya soka ya Yanga umesema kwamba maandalizi kwa upande wao kuelekea kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya JKU kutoka visiwani Zanzibara yamekamilika.

Kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kiujumla kila kitu kwa upande wao kimekamilika kwani wao ndio wameratibu mchezo huyo utakaopigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Amesema kwamba viingilio katika mchezo huo ni shilingi elfu tano kwa majukwaa ya mzunguko huku kiingilio cha juu ni shilingi elfu kumi kwa majukwaa ya VIP.


Hata hivyo Baraka amesema kwamba mechi hiyo ni maombi ya kocha mkuu George Lwandamina ambapo nia yake ni kupata fursa ya kuwaona vizuri wachezaji wake huku pia ni mahusisi kwa ajili ya kumuaga mchezaji Mbuyu Twite anayemaliza mkataba wake.

No comments