SURE BOY ASHIKA SIRI YA UBINGWA AZAM

Na,Said Ally,Zanzibar
Uongozi wa klabu ya Azam FC,umesema kwamba ushindi wa jana wa bao 1-0 mbele ya Singida United ni zawadi kwa mchezaji Abubakary Salum kutokana na mchezaji huyo kufiwa na mama yake mzazi.

Msemaji wa timu ya Azam FC,Jafari Idd amesema kwamba kwa kutambua mchango wake uongozi umeona ni vyema ukamfariji kupitia ushindi huo ambao umewapeleka katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi.

Aidha katika hatua nyingine Jafari alisema kwamba kwa sasa kikosi hicho kinajipanga na mchezo wao wa fainali utakaopigwa siku ya jumamosi dhidi ya URA na anaamini watafanikiwa kuibuka na ushindi katika fainali hiyo kwani dhamira yao ni kutetea taji la michuano hiyo.

Hata hivyo aliongeza kwa kusema kuwa nia yao ni kuendelee kumfariji Sure Boy, hivyo watahakiksha wanafanikiwa kuwa mabingwa wa kombe hilo ili liendelee kuwepo katika ardhi ya Tanzania kwani si vyema taji hilo likaenda nje ya nchi.

No comments