KOCHA YANGA AWAPA PONGEZI REHA FC

 Na Said Ally
Kocha msaidizi wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa amesema kwamba haikuwa kazi nyepesi kwa timu yake kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Reha FC,ambayo inashiriki ligi daraja la pili.

Nsajigwa alisema kwamba kikosi chake kimepata upinzani mkali toka kwa wapinzani wao ambao kwa muda wote walikuwa wanacheza kwa tahadhari kubwa.

Alisema kwamba kwa mfumo wa soka la hapa nchini idadi kubwa ya wachezaji wanafana viwango vyao iwe kwa wachezaji wa ligi kuu ama wa madaraja ya chini na ndio maana si ajabu kuona timu ndogo inapata matokeo mazuri kwa timu kubwa.

Hata hivyo Nsajigwa aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa bidii na kufanikiwa kuchomoza na ushindi huo wa mabao 2-0 ambayo yamewapeleka katika hatua ya 32 bora ya michuano ya kombe la Azam Sport Federation.

No comments