AJIBU KUIKOSA MECHI YA MBAO FC

Na Said Ally
Yanga itamkosa mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya timu ya Mbao FC,mchezo unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza siku ya jumapili.

Msemaji wa timu hiyo,Dismas Ten amesema kwamba Ajibu ataukosa mchezo huo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano ambazo alizipata katika michezo ya awali ya ligi hiyo.

Alisema kwamba mbali na Ajibu wachezaji wengine ambao watakosekana katika mechi hiyo ni pamoja na Thabani Kamusoko,Donald Ngoma na Kelvin Yondani ambao hawa kwa pamoja wote watakosena kwa kuwa ni majeruhi.

Aidha alisema kwamba kikosi hicho kinataraji kuanza safari ya kuelekea Mwanza wakati wowote kuanzia sasa kikiwa chini ya kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa baada ya kocha mkuu George Lwandamina kupatwa na msiba wa kufiwa na mwanae mzazi wiki iliyopita.

Hata hivyo Dismas amewaomba wanachama wa klabu hiyo na mashabiki kuendelea kuisapoti timu yao ili iendelee kufanya vizuri katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara na mashindano mengine ambayo wanashiriki.

No comments