Harakati za klabu ya Mbeya city za kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Burundi Didier Kavumbagu zimegonga mwamba, baada ya pande hizo mbili kushindwa kuafikia makubaliano.

Kavubagu ambaye mkataba wake na klabu ya Azam FC umefikia kkomo tangu mwishoni mwa msimu 2016-17, alikua akihitaji kiasi kikubwa cha pesa kama ada yake ya usajili, hatua ambayo ilionekana kuwashinda viongozi wa Mbeya City.

                                     Didie Kavumbagu

Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema maamuzi ya kuachana na usajili wa mshambuliaji huyo yamefikiwa jana mara baada ya kikao kilichofanyika hadi saa tatu usiku, na sasa wanaangalia uwezekano wa kufanya usajili wa mshambuliaji mwingine ambaye atatokana na orodha waliyonayo.
                                 

No comments