YANGA IKO KAMILI KUWAVAA MO BEJAIA HAPO KESHO







Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara,timu ya soka ya Young Africans umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kipo vizuri kuelekea katika mechi yao ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Mo Bejaia  ya nchini Algeria


Mkuu wa mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amesema kwamba wachezaji wote wana molali ya hali ya juu kuelekea kwenye pambano hilo linalotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Unite Maghrebine

Hata hivyo Muro amewataka watanzania wote kwa pamoja kuelekeza nguvu zao kwa timu hiyo ambayo ni timu pekee ya ukanda wa Afrika mashariki na kati iliyosalia kwenye michuano mikubwa ya ngazi ya vilabu barani Afrika

No comments