MENEJA WA SALUM TELELA AKARIBISHA OFA KWA TIMU ITAKAYOMUITAJI MCHEZAJI HUYO







Meneja wa mchezaji Salum Telela,Shiru Ngushiwa amesema kwamba mchezaji huyo atarejea uwanjani endapo kama itajitokeza timu yeneye ofa nzuri kwa ajili ya mchezaji huyo

Amesema kwamba kwa sasa bado hakuna ofa yeyeote ambayo imejitokeza kwa ajili ya kumsajili hivyo milango ipo wazi kwa timu ambayo ina muhitaji

Amedai hatua hiyo imetokana na uongozi wa klabu ya Yanga kushindwa kumuongeza mkataba mpya mara baada ya mkataba wake kumalizika na taarifa zinadai kua kocha mkuu wa klabu hiyo amependekeza kuachwa

Hata hivyo amedai kua kama hakutatokea timu yenye ofa nzuri basi mchezaji huyo atarejea darasani kwa ajili ya kuendelea na masomo

No comments