Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro,umesema kwamba kwa sasa wapo kwenye wakati mgumu wa kuweza kuwasawishi wachezaji wao ili waweze kusalia kunako klabu hiyo kutokana na namna baadhi ya vilabu vikubwa vya hapa nchini kwa pamoja wote kuelekeza nguvu zao kwa wachezaji hao wakiwa na lengo la kuwasajili



          Shiza Kichuya mmoja wa wachezaji wa Mtibwa Sugar anaewaniwa na klabu ya Simba


Msemaji wa Timu hiyo Tobiasi Kifaru amesema kwamba kwa sasa baadhi ya wachezaji nyota wameshasajiliwa na timu nyingine ikiwemo Simba na Yanga na bado wanaendelea na jitihada za kutaka kusajili wengine hivyo kuendelea kuwaweka kwenye wakati mgumu wakata miwa hao wa Manungu

Kifaru amesema kwamba licha idadi kubwa ya wachezaji kusajiliwa na timu nyingine lkn kwa upande wao hawana kikwazo chochote juu ya kuondoka kwao kwani wana imani timu hiyo nafasi kubwa ya kuibua wachezaji bora




No comments