IHEFU FC WAJINASIBU KUIFUNGA YANGA

Uongozi wa timu ya Ihefu FC umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuwakabili Yanga hapo kesho katika mchezo wao wa kombe la FA utakaopigwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Meneja wa timu hiyo Zagalo Chalamila amesema kwamba kwa upande wao wanaingia katika mchezo huo kwa dhumuni kubwa la kuchomoza na ushindi mbele ya Yanga.

Chalamila alisema kwamba katika mchezo huo anaamini timu yake itaibuka na ushindi na kuisukuma Yanga iende kuungana na Simba ili waendelee na majukumu yao katika ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments